Lava Lava – Tukaze Roho Lyrics

Lava Lava – Tukaze Roho Lyrics

Loading...

Mmmh mmmmh mmmh ;;;

Spice music

Maisha yangu si ya ki papa

Ni vitembele ya nyanya chungu

Dagaa kurusungu, hummh

Niko chakavu na nimechakaa Yaani naishi ki mungu mungu

Mtetezi wa bunjuu

Mjukuu wa binti simba Okoa mangala

Wa mwisho kitinda mimba Mwenye elimu uchwara

Maisha yalivyo nifilimba, akanijalia jallah

Nikaanza kuimba, uniondoke ufukara

Ila bado,

Kipato changu cha chini nacho kina utata

Hata visenti hamsini kuvipata mashaka

Nalia na umasikini mungu ashushe baraka

Enyi wezangu na mimi tusikate tamaa

Tukaze roho, tukaze roho tusichoke

Tukaze roho ,mungu wa kwetu sote

Tukaze roho, eeh  tusichoke

Tukaze roho, mungu wa kwetu sote

Mmh Japo,

maisha yenye ya manati Hatupati kila tukilenga

Kukicha misumari ya bati Kuku kapenya kwa tenga

Kula yetu tu ni wasiwasi Tutapata wapi ya kujenga

Wa kupiga picha masaai Kulala mbagala kwa chemba

Tunaunga unga mwana (haya ndo mambo yetu)

Hayana tofauti na jana(ndo maisha yetu)

Wazazi kulala na mwana(heey…)

Chumba kimoja mandoo, masufuria (wenyewe tushazoea)

Kipato changu cha chini, nacho kina utata

Ata visenti hamsini kuvipata mashaka

Nalia na umasikini mungu ashushe baraka

Enyi wezangu na mimi tusikate tamaa

Tukaze roho, tukaze roho tusichoke

Tukaze roho, mungu wa kwetu sote

Tukaze roho, eeh  tusichoke

Tukaze roho, mungu wa kwetu sote

Iyo lizer

Wanangu wa bodaboda, tukaze roho

Kina mama vikoba, tukaze roho

Ah rumbesi wabeba virogha, tukaze roho

Vijana wezangu, tukaze roho Tutapata tu

Similar Posts:

Leave a Reply

Close Menu